Kilimanjaro Stars kamili kushiriki kombe la Mapinduzi

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars, Ahmad Ally ametangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano mipya ya kombe la Mapinduzi itakayofanyika katika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.

Mbali ya kuita nyota wapya, baadhi ya wachezaji ambao wamekuwa wakiitwa mara kwa mara kwenye timu ya taifa ya Taifa Stars wamejumuhishwa pia.