Ramovic amtosa Makame Yanga
Kocha Sead Ramovic ameukataa usajili wa mlinzi wa kati wa Fountain Gate FC, Laurian Makame baada ya kumtazama kwenye mchezo kati ya Fountain Gate FC dhidi ya Azam FC.
Uongozi wa Yanga ulikuwa ushafanya kila kitu ili Laurian Makame ajiunge na Yanga ila imeshindikana baada ya Ramovic kumkataa, Kama mwalimu angekubali usajili wake basi mchezo wa jana asingekuwa sehemu ya kikosi cha Fountain Gate FC bali angekuwa ndani ya Yanga.
Dili lake lilikuwa asilimia 90% linakwenda kukamilika.