Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC imekuwa ya moto zaidi baada ya kuilaza Fountain Gate mabao 5-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam.
Pacome Zouzoua dakika ya 15 alifungua akaunti ya mabao kabla ya Mudathir Yahya dakika ya 40 kufunga bao la pili, moto wa Yanga uliendelea tena pale Zouzoua alipofunga bao lake la pili kwa mchezo wa leo na la tatu kwa Yanga dakika ya 45.
Mabingwa hao wa bara waliandika bao la nne dakika ya 51 kupitia kwa Jackson Shiga aliyejifunga, Clement Mzize dakika ya 87 alifunga bao la tano na la sita kwake.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 39 nyuma ya Simba yenye pointi 40 zikifukuzana kileleni