CS SFaxien yaadhibiwa na CAF


Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limeitoza faini ya dola 50,000 (Zaidi ya milioni 120 za Kitanzania) timu ya CS Sfaxien ya Tunisia, pamoja na adhabu ya kucheza mechi mbili za nyumbani za kombe la shirikisho bila mashabiki.

Mechi hizo zitakuwa ni dhidi ya Simba SC na FC Bravos ya Angola, adhabu hiyo imetolewa baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Simba uliochezwa December 15 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.