Kikosi cha Wanalambalamba Azam FC usiku huu wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu bara.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Paschal Msindo na Iddi Nado aliyefunga mabao mawili, bao pekee la kufuta machozi la JKT Tanzania lilifungwa na Juma.
Kwa ushindi huo Azam FC imefikisha pointi 36 ikilingana na Yanga yenye pointi 36.