Mtangazaji wa kituo cha redio cha Magic Fm, Sunday Mwakanosya amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinasema Mwakanosya amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi.
Enzi za uhai wake Mwakanosya alikuwa akitangaza kipindi cha muziki wa dansi na alikuwa mdau mkubwa wa muziki huo.
Mungu aipumzishe roho yake mahara pema peponi.