Simba yazidi kuunusa ubingwa

Lilikuwa ni bao la dakika ya 90 na ushei la mkwaju wa penalti wa Kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua aliyemchambua kipa Yacoub Suleiman wa JKT Tanzania baada ya beki Mohamed Bakari kumchezea rafu Shomari Kapombe kwenye boksi.

Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukaa kileleni kwakufikisha pointi 37 na mwishoni mwa wiki hii itaumana na Singida Black Stars.

Pia goli la Ahoua linamfanya afikishe mabao 7 kumsogelea kwa karibu kinara wa mabao Elvis Rupia mwenye mabao manane