Baleke atoboa siri kinachomweka benchi Yanga
Kupitia Ukurasa wake Tiktok Live, Jean Baleke alisema moja kati ya sababu kubwa ya kutofautiana na Uongozi wa Yanga ni suala la malipo ambayo yamechelewa kwa kipindi kirefu kidogo jambo ambalo lilimfanya ashindwe kutumika vizuri.
“Nilipewa barua wiki iliyopita na kwangu naona ni uamuzi mzuri tu ambao klabu imefikia kwani sikuwa napata haki yangu kama ilivyotakiwa. Sijalipwa mshahara wangu miezi miwili, suala ambalo sio zuri kwa upande wangu, niko tayari sasa kwa changamoto mpya