YANGA Princess imekamilisha uhamisho wa mlinzi wa kushoto Diana Mnally kutoka Gates Program.
-
Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa imani yao ni kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Simba Queens atakuwa sehemu ya mafanikio yao.
-
Msimu uliopita Diana aliachana na Simba Queens na kujiunga Gates Program lakini sasa amepata malisho mapya huko jangwani.
-
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya wanawake anaingia katika orodha wa wachezaji wa kike waliokipiga Simba na Yanga, wengine ni Amina Ally, Precious Christopher, Saiki Atinuke, Danai Bobo,Wema, Daniella Ngoyi nk.