Jeshi la Magereza latoa onyo kwa wanaolibeza

Uongozi wa Jeshi la Magereza limetoa onyo na kuwataka kuacha kutoa kauli zenye mwelekeo wa kubeza au kudharau Mamlaka yake.

Kauli hiyo imetolewa na Msemani wa Jeshi la Magereza baada ya kipande cha video kilichosambaa mtandaoni kikimuonesha, Ndugu Haji Manara kukataa kwa dharau na kuanza kutoa maneno yasiyo ya kiungwana baada ya kuombwa kutoa gari lake mbele lililozuia gari la Jeshi la Magereza.