Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars leo wamesafiri kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi itakafanyika uwanja wa Gombani, Zanzibar.
Mapema leo wachezaji hao na benchi lake la ufundi chini ya Ahmad Ally, wakiwa bandarini walianza safari kuzifuata timu nyingine za taifa kushiriki michuano hiyo mipya.