Hussein Massanza aibeza Simba na kuwaita akademia

Msemaji wa timu ya Singida Black Stars ya mkoani Singida, Hussein Massanza ni kama amewabeza Simba SC kwa kudai kwamba imesajili wachezaji vijana hivyo ni akademia.

Msemaji huyo amedai kwamba katika mchezo wao wa kesho katika uwanja wa Liti, Simba SC wasitegemee kubebwa kwa kupewa penalti isipokuwa watafungwa zaidi ya goli moja kwakuwa wanao wachezaji wazuri wa kumaliza mechi.

'Nawaona Simba SC kama academy kwa sababu wamekusanya vijana wengi wadogo wadogo kama wapo kwenye majaribio"

Simba SC ni timu yenye mipango hata sisi tunaijua na tutapita humo humo kwa sababu mechi tunaitaka"

Alisema Hussein_Massanza
Msemaji wa klabu ya Singida Black Stars.

Hussein Massanza