Mchezaji wa Chelsea mbioni kutua Simba

Kiungo mshambuliaji raia wa Ghana na klabu ya Berekum Chelsea Stephen Amankona yupo katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Simba Sc katika dirisha hili dogo la usajili

Amankona anatarajia kuanza safari kuja nchini Tanzania kumalizia sehemu ya makubaliano yaliyosalia ili kukamilisha dili hilo la kujiunga na Simba

Kiungo mpaka sasa kwenye klabu yake kafanikiwa kufunga magoli 5 katika michezo 12 aliyocheza Hana Assisti