Ramovic amfunika Gamondi
Kocha mkuu wa Yanga Saed Ramovic amekuwa na takwimu bora sana tangia ajiunge na Yanag tofauti na mtangulizi wake Miguel Gamondi.
Hadi hivi sasa Ramovic ameiongoza Yanga kwenye michezo minne ya Ligi, timu yake imefunga magoli 13 imefungwa magoli mawili tu .
Miguel Gamondi ameiongoza Yanga kwenye michezo kumi msimu huu , timu yake imefunga magoli 14 na kufungwa magoli manne .