Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Pacome Zouzoua ameweka wazi kuwa kocha Saed Ramovic ni mkali sana hataki kabisa mchezaji akae na mpira kwa muda mrefu akiwa uwanjani.
“Kocha ni mkali sana.Hataki ukae na mpira mguuni muda mrefu.Anataka twende mbele kwa kasi yaani gusa tuondoke.Tumeona mabadiliko makubwa sana.Mbinu zake na mifumo yake inataka uwe na pumzi ya kutosha."
"Hataki kuona kabisa unakaa na mpira hata sekunde tano.Ukiupata unatakiwa kujua unaupeleka wapi na kwenda kuunda umbo wapi.Kifupi tukabe wote, tufunge wote.“
Pacome Zouzoua, kiungo wa klabu ya Yanga.