Mwanamuziki wa dansi Tabia Batamwanya ameguswa na kifo cha aliyekuwa mtangazajj wa Magic Fm, Sunday Mwakanosya kilichotokea jana katika hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila.
Akizungumza kupitia kurasa yake ya Facebook, Batamwanya ameguswa na msiba huo akidai ni pigo kubwa kwa muziki wa dansi kwani marehemu alikuwa na mchango mkubwa.
"Namfahamu kwa muda mrefu marehemu Sunday, sina la kusema zaidi ya kumtakia mapumziko mema peponi Amina" alisema Batamwanya ambaye ni mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa dansi