Kutoka Yanga hadi KVZ


Klabu ya Soka ya KVZ FC imefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji nyota raia wa Tanzania Yohana Mkomola (24) na kumsainisha mkataba wa Miaka 2 kuhudumu ndani ya klabu yao.

Ikumbukwe Yohana ambaye alishawahi kuhudumu katika kikosi cha Tabora United ni miongoni mwa wale Nyota kizazi cha Dhahabu cha wakina Dickson Job, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage na Wakina Ramadhani Kabwili.

Pia aliwahi kuichezea Yanga SC kabla ya kutimkia Ukraine.

Akiwa FIT Mkomola ni miongoni mwa Vipaji hatari sana na wanauwezo mkubwa sana wa kuiweka safu ya timu pinzani matatani, naamini hapa KVZ wamepata mtu haswa na atawasaidia.