Timu ya Tanzania Prisons ya Mbeya jioni ya leo imeichapa Pamba Jiji FC ya Mwanza bao 1-0 katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mchezo wa Ligi Kuu bara.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Tariq Abdallah Simba aliyefumua shuti la umbali wa mita 17 kumtungua kipa wa zamani wa Tanzania Prisons, Yona Geoffrey Amos dakika ya 31.