Timu ya Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, jioni ya leo wameifunga timu ya Dodoma Jiji mabao 4-0 na kuendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya watani zake Simba.
Ikicheza kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Yanga iliandikisha mabao yake kupitia kwa Clement Mzize aliyefunga mawili, Stephanie Aziz Ki na Prince Dube.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 36 ikizidiwa pointi moja tu na mtani wake Simba yenye pointi 37, Jumapili Yanga itaumana na Fountain Gate.