Mwanachama maarufu wa Klabu ya Yanga SC, Haji Manara, ameomba radhi kwa mara nyingine kwa Jeshi la Magereza, Kamishna Mkuu, viongozi wa jeshi hilo na askari wake wote kufuatia sakata lililotokea siku ya mechi ya Yanga SC vs Tanzania Prisons katika Uwanja wa KMC.
Manara ameweka wazi kwamba hana maneno yanayoweza kuzidi neno "Samahani", akisisitiza kuwa mazungumzo yake ya awali yalitokana na hisia za kishabiki. Pia amesisitiza heshima yake kubwa kwa Jeshi la Magereza na taasisi nyingine za dola nchini.
"Heshima yangu kwa taasisi hii muhimu haiwezi kuwa na mbadala wa neno samahani," amesema kwa unyenyekevu mkubwa.