Klabu ya AmaZulu ya Ligi Kuu ya Soka Afrika Kusini imetuma ofa kumsajili Mshambuliaji wa Simba SC ya ligi kuu Tanzania Bara, Kibu Denis (26).
AmaZulu imefanya mazungumzo na Wekundu wa Msimbazi kuhusu Kibu,
AmaZulu FC iliyochini ya kocha Pablo Franco Martin aliyewahi kuwa kocha wa Simba SC tangu 2021 - 2022,
AmaZulu katika msimu huu wa ligi kuu soka Afrika Kusini inashika nafasi ya 13 kwa alama 9 ilizovuna kwenye michezo 9.
Msimu uliopita ilifanikiwa kumaliza nafasi ya 11 kwenye ligi kuu ikiwa na alama 36 katika michezo 30.