Namungo yaituliza Fountain Gate

Timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi mchana wa leo imewafunga mabao 2-1 timu ya Fountain Gate katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara mchezo wa Ligi Kuu bara.

Mabao ya Namungo FC yamefungwa na viungo Pius Charles Buswita dakika ya 10 na Geoffrey Julius Luzendaze dakika ya 78, wakati bao pekee la Fountain Gate limefungwa na winga Salum Kihimbwa dakika ya 30.

Fountain Gate mwishoni mwa wiki hii itaumana na mabingwa watetezi Yanga SC katika kuwania pointi tatu muhimu