Ahmed Ally alia na kocha wa Dodoma Jiji

Baada ya Yanga SC kushinda mchezo wa Ligi kuu Soka Tanzania bara dhidi ya Dodoma Jiji kwa magoli 4-0, Meneja wa habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally kupitia mtandao wake wa Instagram amemtupia lawama Kocha wa Dodoma Jiji Mecky Mexime juu ya kauli zake.

Ahmed Ally ameandika kuwa ''Dodoma Jiji jana kafungwa magoli mawili ya Uwongo, Moja la Offside na pili Penati ya uongo lakini Kocha wao hajalalamika kuonewa wala kudhulumiwa zaidi amesema

AMESTAHILI KUFUNGWA.

Rejea mechi ya Dodoma Jiji Vs Simba, baada ya sisi kufunga goli la Penati ya halali alitoa mapovu kulaumu Waamuzi yote ni kuaminisha watu kuwa tumemdhulumu na kutaka kutia dosari kazi nzuri inayofanywa na Simba Sports msimu huu.
Nimeyasema haya ili Wana Simba tuone vita ni kubwa iliyombele yetu ni namna gani Wapinzani hawapendi kufungwa na sisi lakini wanafurahi kufungwa na wengine, ndio maana haishangazi kuona tunapata ushindi wa jasho na damu''

''Wale wanaosema tunashinda lakini tunashikilia roho sio kwa sababu tuu ya ubora ni kwa sababu wapinzani wanauma meno kupitiliza na sisi ndio tunapenda ushindani wa aina hiyo,

Kuelekea mechi zijazo Wana Simba tunapaswa kuunganisha nguvu kweli kweli, tupambane kwa nguvu sawa kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.''- Amesema Ahmed Ally akitupa lawama kwa Mexime