Timu ya Singida Black Stars leo mchana imeifunga KenGold mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Liti mjini Singida.
Kwa matokeo Singida Black Stars imefikisha pointi 33 ikiendelea kushika nafasi ya nne nyuma ya Azam FC, KenGold walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Herbery Lukindo dakika ya 26.
Lakini Josephat Arthur aliifungia Singida Black Stars bao kwanza dakika ya 46 na la kusawazisha, kabla ya Elvis Rupia dakika ya 56 kufunga bao la ushindi.
Kipigo hicho kwa KenGold kimeifanya timu hiyo izidi kuchungulia kaburi la kushuka daraja, Singida sasa itaumana na Simba mwishoni mwa wiki