Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2025

Kimenuka huko CAS, Bodi ya Ligi, TFF na Simba zapewa siku 10

Bodi ya Usuluhishi wa Kesi za Kimchezo ya CAS imethibitisha kupokea barua ya Yanga ambapo Walalamikiwa ni TFF, BODI na SIMBA. Walalamikiwa wamepewa siku 10 baada ya kupokea taarifa rasmi kutoka CAS kuanza kuandaa utetezi wao wakati mchakato wa kesi unaanza rasmi kusikilizwa kwa nyaraka yenye kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298.

Kocha wa Yanga kuipangia kikosi cha kwanza Tabora United

KOCHA wa Yanga, Hamdi Miloud, amesema anahitaji kuingia na kikosi cha ushindani katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tabora United, akisisitiza umuhimu wa kupata ushindi. - Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumatano, Aprili 2, kwenye Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, Tabora. Yanga inakwenda katika mechi hiyo ikiwa na morali baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa kuiondoa Songea United. - Kocha Hamdi amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma katika mchezo dhidi ya Songea United na kueleza kuwa maandalizi ya mchezo ujao yanaendelea kwa nguvu. - Ameongeza wanatambua changamoto ya kucheza ugenini, hasa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza walipokutana na Tabora United, lakini wanajipanga kulipa kisasi.

Mbeya City yamtambulisha Malale Hamsini

Timu ya Mbeya City (Wanakoma Kumwanya) ya jijini Mbeya imemtambulisha Malale Hamsini kuwa kocha wao mpya, akichukua nafasi ya Salum Mayanga aliyekwenda kuifundisha Mashufaa FC. Kazi kubwa inayomkabili kocha Malale Hamsini ni kuhakikisha Mbeya City inarejea Ligi Kuu msimu ujao. Kwa sasa, Mbeya City inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ikiwa na alama 55 baada ya michezo 25, ikizidiwa alama tano na Mtibwa Sugar, huku zikiwa zimesalia mechi tano pekee. Malale Hamsini, mzawa wa Zanzibar, ana uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania Bara, kwani amewahi kufundisha zaidi ya timu tatu za Ligi Kuu, huku timu yake ya mwisho ikiwa JKT Tanzania.

Yanga hatuna mechi ngumu Jumatano - Alikamwe

Msemaji wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe amesema mechi yao ya Jumatano dhidi ya Tabora United itakayofanyika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi itakuwa nyepesi na wala si ngumu ila kuna watu wanataka kuiona ngumu. "Kiukweli kabisa wa mpira Jumatano sisi Yanga SC hatuna mechi ngumu hapa Tabora ila wapo watu wachache kwasababu zao sijui za kisiasa wanataka kukaa mbele wazungumze wasikike na waonekane hao ndio wanawaaminisha watu kuwa jumatano Ally Hassan Mwinyi kutakuwa na mchezo mgumu kwelikweli huo ni uongo." . "Sisi Yanga tuna muheshimu sana Rais Samia ila huyu mtu wake aliyemtuma huku Tabora anatuchokonoa anatutafuta la rohoni sisi Yanga, Kiheshima tunamuomba radhi kwanza aliyemtuma halafu Yanga tunashuhulika nae, tumwambie mkuu wa mkoa Paul Chacha jumamosi atachacha kweli." . Amesema Ally Kamwe Meneja Habari wa Klabu ya Yanga SC.

Iliniuma sana Prince Dube kuhama Azam FC kwenda Yanga- Zakazi

Afisa Habari wa klabu ya Azam FC Zackaria Zakazi " Zaka Zakazi" amesema hakuna kitu kinachomuuma kama mchezaji Prince Dube aliyekuwa Azam FC kuhamia Yanga. "Nilimuita mwanangu jina la Prince kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga mwaka 2021 halafu Prince Dube akafunga goli karibu na katikati ya uwanja,jambo lililonifurahisha sana ndio maana nikasema kwa heshima hiyo nimpe mwanangu jina lake" "Kwa sasa nimembadilishia jina kwa sababu sifurahii tena kumuita Mwanangu Prince tangu Prince Dube alipoondoka Azam" . ZAKA ZAKAZI,Afisa Habari wa Klabu ya Azam FC. Zakazi akiwa na Dube aliyevaa jezi ya Azam

Zamalek walia na udhalimu wa Al Ahly

Klabu ya Zamalek ya Nchini Misri imepinga uamuzi wa Chama cha vilabu Nchini humo kuhusu kutenguliwa kwa adhabu dhidi ya Al Ahly ikiitaja hatua hiyo kuwa ni kama udhalimu kwenye mpira. Haya yanajiri baada ya Chama cha vilabu kutangaza kuwa Al Ahly hawatakatwa pointi tatu mwishoni mwa msimu ingawa Zamalek watapatiwa pointi tatu baada ya Al Ahly kugomea kupeleka timu uwanjani kwenye mchezo baina ya timu hizo. Hata hivyo Zamalek imepinga vikali hatua hiyo kwa kile ilichodai ni kutojali maslahi ya mashabiki wa thamani wa timu hiyo na haitaridhia kudhulumiwa haki yoyote huku wakitaka Ahly apokwe alama kama awali na wao kupewa ushindi huo kikanuni kama kawaida.

Nyuma ya Fadlu huyu jamaa hatari

Nyuma ya kocha mkuu Fadlu Davids kuna huyu mwamba wakuitwa Darian Wilken akishilikiana na Sulemani Matola wanafanya kazi kubwa sana. Darian Wiliken amemaliza sehumu ya pili ya ukocha UEFA A License aliyokuwa anasoma Wales. hivyo kwasasa yuko fiti kusafiri na Simba kuelekea nchi ya Hadi.

Mnoga aisaidia Salford City Ligi daraja la pili Uingereza

Nyota wa Tanzania Haji Mnoga ameisaidia timu yake ya Salford City kupata alama tatu akitoa pasi ya usaidizi (Assist) katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bromley katika mchezo wa Ligi ya Pili (League Two) ya Uingereza

Mufti mkuu Tanzania aweka wazi kesho Eid Mubarak

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ametangaza kuwa mwezi umeonekana katika maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani hivyo kesho Jumatatu March 31,2025 itakuwa ni Sikukuu ya Eid Al Fitri. Akitangaza Jijini Dar es salaam leo, Mufti Zubeir amesema “Nawatangazia Waislamu wote kuwa mwezi umeandama na umeonekana na kushuhudiwa sehemu nyingi katika nchi yetu, pia umeonekana Kenya, Pemba na Arusha wameona waziwazi mwezi, hivyo nimeuthibitisha mwezi huo na kesho itakuwa Eid”

Azam FC kuachana na kipa wake tegemeo

Kama mambo yataenda kama yalivyo, Azam FC ina mpango wa kumtema kipa wake Mohamed Mustafa raia wa Sudan sababu ikitajwa ni kufanya makosa mengi akiwa golini, hivyo umeanza mchakato wa kumsaka mbadala wake atakayewasaidia msimu ujao. Chanzo cha ndani kutoka Azam FC kinasema tayari uongozi wa timu hiyo umcanza mazungumzo na kipa namba moja wa As Vita ya DR. Congo. Farid Ouedraogo na kama dili likitiki basi Mustapha atapewa mkono wa kwaheri

Yanga na Rayon kuzindua uwanja wa Amahoro

Rais wa Klabu ya Rayon Sports ya Nchini Rwanda Twagirayezu Thaddee amethibitisha kuwa Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa ipo tayari kucheza nao kwenye mchezo wa kirafaiki katika uwanja mpya wa Amahoro kujiandaa na Msimu mpya wa Mashindano wa 2025/26. Pia kwasasa Klabu ya Rayon Sports ambao ni kinara wa ligi kuu ya Rwanda na ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu mbele ya APR. Rayon Sports ipo chini ya Kocha wa zamani wa klab ya Simba Raia wa Brazil Oliveira Roberto ' @robertinho7.coach Kwa mujibu wa moja ya Chapisho la Michezo kutoka Nchini Rwanda lilianduka kuwa Uongozi wa klab ya Rayon Sports licha ya Raisi wa klab yao kuwa na Ukaribu mzuri na Raisi wa klab ya Young Africans Hersi Said pia klab ya Yanga ni miongoni mwa Vilabu pendwa kwasasa Nchini Rwanda na Afrika. Young Africans ndio Vinara wa ligi kuu ya Tanzania na ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu huu.

Wydad Casablanca yabisha hodi Jangwani, kumchomoa Aziz Ki

Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco inafuatilia kwa umakini mwenendo wa Stephanie Aziz Ki kuangalia muafaka na utaratibu wa kupata saini yake..... Wydad imekua ikimfuatilia kwa muda sasa wa miaka 2 ili waangalie uwezekano wa kumpata kiungo huyo... Kocha wa Wydad ndie anaeongeza shinikizo zaidi la kumpata KI, anavutiwa sana na uchezaji wake. Hatua za awali zimeshaannza kujadili juu ya uhamisho wake, jana wawakilishi wa Aziz Ki walikutana na kocha Rulani Mokwena na klabu staff wa Wydad

Kesho ni Eid Mubarak Saudi Arabia

Saudi Arabia wametangaza Mwandamo wa Mwezi jamba ambalo linaashiria kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kesho Jumapili ni Eid Al Fitr. Kwa upande wa Tanzania tayari Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr inatarajiwa kuwa Machi 31 au Aprili mosi, kulingana na mwandamo wa mwezi. Sherehe za kitaifa zitafanyika jijini Dar es Salaam ambapo Swala ya Eid itaambatana na Baraza la Eid litakalofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere saa 9 Alasiri. Mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamba Jiji hiyooo robo fainali kombe la CRDB

Klabu ya Pamba Jiji kutoka Jijini Mwanza imeibuka na ushindi Wa Bao 1-0 Dhidi ya klabu ya Mashujaa Fc ya Mkoani Kigoma katika mchezo Wa hatua ya 16 Bora ya Michuano ya CRDB Federation Cup mchezo ambao umepigwa majira ya Saa 10:00 Jioni katika dimba la Lake Tanganyika Mkoani Kigoma. Bao la Pamba Jiji limefungwa na nyota wao Allan Mukeya na kuifanya Pamba Jiji kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo.

Yanga yaifuata Simba robo fainali kombe la CRDB Cup

Mabingwa watetezi wa kombe la CRDB Cup, Yanga SC jioni ya leo wameifunga Songea United ya mkoani Ruvuma mabao 2-0 uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam. Mabao ya Duke Abuye dakika ya 21 na Jonathan Ikangalombo dakika ya 54 yametosha kuipeleka hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake anakwenda kushiriki kombe la Shirikisho barani Afrika.

Gibrili Sillah kuongeza mkataba Azam FC

Azam FC na Gibrill Sillah watakaa mezani mwezi wa 4 (siku 2 zimesalia) kujadili hatma ya Mchezaji huyo ambaye mkataba wake wa sasa unaisha mwishoni mwa msimu huu 2024/25. Sillah aliuomba Uongozi wa Azam FC umuache mpaka itakapofika mwezi wa 4 mwaka huu ndipo afanye maamuzi, alitaka muda wa kuutumikia mkataba wake wa sasa na hakutaka kufikiria chochote kingine. Kuna timu 2 za Ulaya (Ufaransa na Ubelgiji) ambazo zinamuhitaji Gibrill Sillah, lakini pia Wydad Casablanca nao pia wameshafanya mawasiliano na Wakala wa Sillah. Hakuna timu yeyote ya Tanzania ambayo imeshafanya mawasiliano na Gibrill Sillah wala Wakala wake.

Ombi la Pyramids kuchezeshwa na waamuzi wa nje dhidi ya Al Ahly lakubaliwa

Ombi la klabu ya Pyramids kutaka waamuzi wa nje kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi vs Al Ahly limekubaliwa kutekelezwa na Chama cha Soka EFA huku kukiwa bado hakuna majibu ya ikiwa Al Ahly itacheza mchezo huo! Pyramids waliwasilisha Maombi Yao na watalipa gharama za waamuzi hao punde baada ya sherehe za Eid zinazotarajiwa kufanyika Kesho au keshokutwa nchini Misri

Kingwendu aomba anunuliwe gari na Diamond Platinumz

Msanii mkongwe wa Filamu Nchini Tanzania Kingwendu amemuomba Msanii Diamond Platnumz amnunulie Gari kwa sababu anapata changamoto sana ya Kiusafiri Kingwendu amesema alipojiingiza kwenye siasa alipata madeni makubwa, hali iliyopelekea kutetereka kiuchumi na kuuza magari yake yote Kingwendu amesema anaishi mbali "Nzasa" na huwa anatumia gharama kubwa ya Usafiri anapotaka kwenda katika kazi zake hivyo Diamond amsaidie Amnunulie hata Gari Aina ya IST. Diamond Platnumz

Morrison aomba muda zaidi wa kurejea fiti

Winga wa KenGold Bernard Morrison amesema licha ya kurejea mazoezini na wenzake lakini bado hajawa fiti kuchèza mechi akiomba muda zaidi kuwa sawa, huku akilia kuikosa Ligi Kuu. Nyota huyo raia wa Ghana alitambilishwa kikosini humo dirisha dogo akiwa huru, ambapo hajacheza mechi yoyote kati ya saba iliyochezwa na timu hiyo kufuatia majeraha ya paja yaliyokuwa yanamsumbua. Kutokana na hali hiyo, benchi la ufundi lilimpa program maalumu ya kujifua kivyake ambapo kwa sasa tayari ameungana na wenzake kujiwinda pamoja kwa ajili ya mwendelezo wa Ligi inayotarajia kuendelea April 3. Nyota huyo akiwa Yanga SC msimu wa 2019/20 alicheza mechi 13 akifunga mabao manne na asisti tatu, ambapo msimu uliofuata alijiunga na Simba SC akiifungia mabao manne na kuhusika mengine saba kati ya mechi 24.

Yanga yaingia mkataba na Kamisheni ya Utalii Zanzibar

Kamisheni ya Utalii Zanzibar imeingia rasmi katikaushirikiano na klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga SC) kwa kusaini mkataba wa kutangaza vivutio vya Zanzibar kupitia kauli mbiu ya “Visit Zanzibar.” Mkataba huo umesainiwa tarehe 28 Machi 2025, na KatibuMtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ndugu Arif Abbas pamoja na Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said, mbele ya mgeni rasmi Mheshimiwa Mudrik R. Soraga, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, ambaye alishuhudiatukio hilo muhimu. Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii, Arif Abbasalieleza kuwa kupitia kampeni ya “Visit Zanzibar” kwenye jezi za Yanga, Zanzibar itanufaika kwa kufikia soko la kutangaza utalii wa ndani “Domestic Tourism”, Utalii wakikanda na bara zima la Afrika kutokana na umaarufu wa timuhiyo na wachezaji wake kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika. Kwa upande wake, Eng. Hersi Said alieleza furaha ya klabuyake kushirikiana na Kamisheni ya Utalii Zanzibar. “Kwa msimu mzima ...

Kagera Sugar ya Juma Kaseja yatinga robo fainali kombe la CRDB

Kagera Sugar ya Juma Kaseja imetinga robo fainali ya Kombe la CRDB kwa kuwaondoa Tabora United kwa mikwaju ya penati 3-5 baada ya sare ya 1-1. Katika dakika 90 za mchezo huo, Tabora United ilitangulia kwa bao la beki wake Mkongo, Andy Bikoko dakika ya tatu, kabla ya kiungo mzawa, Joseph Mahundi kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 28.  Kagera Sugar inaungana na Singida Black Stars, JKT Tanzania, Mbeya City, Stand Utd na Simba SC ambazo zimeshatinga robo fainali ya Kombe la CRDB BANK. Kagera Sugar imebebwa na uzoefu wa wachezaji wake waliokuwa nao, Tabora United licha ya kuwa na wachezaji bora lakini imetupwa nje. Kipa Ramadhan Chalamanda ni shujaa wa mchezo kwa kuisaidia timu yake kutinga robo fainali kwa kuzuia mchomo wa penalti.

Yanga yasisitiza hawachezi dabi

KLABU ya Young Africans imeendelea na Msimamo wa kutocheza Mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Simba mchezo ambao awali ulipangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu. Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa Young Africans Ali Kamwe wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Visiwani Zanzibar mara baada ya kumalizika Kwa utiaji wa saini wa makubaliano baina ya Young Africans na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar, kuhusu kuitangaza Zanzibar kupitia “Visit Zanzibar”.

Simba, Al Masr kucheza kwa Mkapa

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kutumika kwa mechi zote za robo fainali au nusu fainali kwa klabu ya Simba. Awali CAF ilitangaza kuufungia uwanja huo baada ya kutoridhishwa na ukaguzi uliofanywa na wakaguzi wake, kwa maana hiyo sasa Simba itarudiana na Al Masr katika uwanja huo. Tayari Simba ilijiandaa kusafiri Rwanda ama Uganda kwa ajili ya kutumia kama uwanja wa nyumbani baada ya kuzuiwa kwa Mkapa.

Walionunua tiketi za Constantine kuiona Al Masr - Simba SC

Klabu ya Simba imetangaza kuwa mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi za mechi yao dhidi ya Constantine watazitumia kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry ya Misri. Hayo yamebainishwa na Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally Machi 26, 2025. "Wale wote ambao walinunua tiketi dhidi ya Constantine watatumia tiketi zao kwenye mchezo dhidi ya Al Masry." Uamuzi huo umekuja baada ya CAF kuiadhibu Simba kwa kucheza mechi moja bila mashabiki na faini ya dola 40,000 kufuatia vurugu zilizoibuka kwenye mechi yao dhidi ya CS Sfaxien ya Algeria mnamo Desemba 15, 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Diamond Platinumz hataki Tiffah awe msanii kama yeye

Diamond Platnumz amesema hatomruhusu binti yake,Tiffah kuwa msanii kwani anazijua changamoto za kuwa msanii ukiwa mwanamke. "Msanii wa kike kuna mambo mengi lazima apitie kama anataka kuwa msanii, Ni changamoto kubwa sana kiasi cha kuuza mpaka utu lakini ndo mfumo ulivyo." Ameandika kupitia mtandao wake, Diamond Platnumz

Hatujaitwa na Waziri Kabudi kujadili Yanga na Simba - Mangungu

Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu amesema wao hawakuitwa na Waziri Kabudi kwa ajili ya sakata la mechi ya dabi dhidi ya Yanga isipokuwa waliitwa kujadili maendeleo ya soka la Tanzania. Amedai Simba ndio timu pekee inayowakilisha nchi kimataifa hivyo ni wajibu kushirikishwa kwenye mambo makubwa. "Kikao chetu sisi kimejadili maendeleo ya mpira hakijajadili walichojadiana na wenzetu, tungejadili mechi yetu tungeitwa kwa pamoja ila mamlaka si ilishasema mechi yetu itapangiwa tarehe nyingine." "Sisi tumejadili maendeleo ya soka Tanzania, Kikao chetu sisi hakihusiani na chao." Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.

Simba yatangulia robo fainali kombe la CRDB

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wametangulia kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CRDB Cup baada ya kuilaza Bigman- FC mabao 2-1 uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mzambia, Joshua Mutale dakika ya 16 na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 31, wakati bao pekee la Big Man FC limefungwa na Joseph Henock dakika ya 45.

Maxi Nzengeli kusalia Jangwani

Maxi Nzengeli ataongeza mkataba wa miaka miwili ya kuendelea kubaki Ndani ya Yanga SC. Uongozi wa YANGA SC umeanza mazungumzo rasmi na timu AS Maniema Union ili kukamilisha dili hilo Japo kiongozi wa timu ya AS Maniema Union Jenerali Kumba amesema mahusiano mazuri kati ya Yanga na timu hiyo ni makubwa hivyo uhakika wa mchezaji huyu kubaki jangwani ni mkubwa #ngindoupdates || #ngindomedia

Taifa Stars ilijiandaa kufungwa...

Na Prince Hoza MABAO ya Simba wa Atlasi yaliyoizamisha Taifa Stars yamefumgwa na nyota wa La Liga, beki wa Real Sociedad, Nayef Aguerd dakika ya 51' na kiungo wa Real Madrid, Brahim Díaz kwa Penalti dakika ya 58 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Oujda.  Hicho ni kipigo ilichokipata Taifa Stars dhidi ya Morocco, kipigo ambacho kimewasononesha Watanzania wengi, matumaini ya Tanzania kutinga fainali za kombe la dunia yanawekwa shakani na kipigo hicho. Morocco si daraja letu kiasi kwamba kufungwa ni kama dhambi, hapana Morocco ni timu ya kiwango cha juu sana ambapo ni mapema sana kuifikia na kuiweka chini. Malalamiko kufungwa na Morocco yanakuja kwamba hakukuwa na maandalizi hata kidogo kuelekea mchezo nao, Iko tofauti na mechi nyingine Taifa Stars inajiandaa vya kutosha, lakini mechi dhidi ya Morocco hakuna maandalizi kabisa. Nashangaa kuona mchezo mkubwa wa kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Morocco, Taifa Stars inasafiri pasipo hamasa yoyote, nilichokiona kwa Taifa Stars ni sif...

Meddie Kagere na bonge la rekodi bongo

Nyota wa zamani wa timu za Singida Big Stars na sasa Namungo FC raia wa Rwanda, Meddie Kagere 'MKI4', anashikilia rekodi ya kipekee wakati anacheza Simba SC kwa mastaa wa kigeni katika Ligi Kuu Bara, ambayo hadi leo inaishi na wala haijavunjwa. Kagere alitua Simba SC akitokea Gor Mahia ya Kenya msimu wa 2018-2019 na kufunga mabao 23 na kuipiku rekodi ya aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe ya wachezaji wa kigeni kufunga mabao mengi msimu mmoja alipofunga 21 msimu wa 2015-2016. Msimu wa 2019- 2020, staa huyo akiwa na Simba SC pia, alifunga mabao 22 na kutetea tuzo ya mfungaji bora ikiwa pia ni rekodi kwani, haijawahi kutokea kwa mchezaji yeyote iwe mzawa au wa kigeni kuchukua tuzo ya ufungaji bora mara mbili mfululizo.

Simba wakiri kubeba mbuzi na wazee warupi siku ya dabi

Taarifa ya Bodi ya Ligi inasema, walihairisha mechi kwa sababu za Usalama na uwepo wa viashiria vya rushwa..  Simba SC leo viongozi wao wamekiri kuwa kweli Machi 7, 2025, walibeba basi lenye mbuzi na wazee wafupi na kuingia nao uwanjani usiku, walipozuia wakagoma kuleta timu uwanjani Kimsingi, Wanachokifanya @simbasctanzania ni kuzidi kuwavua nguo viongozi wa Bodi ya Ligi @yangasc wako sahihi, Mpira wetu unaongozwa na watu wa hovyo kuwahi kutokea. Nitawashangaa sana Viongozi wa Yanga kama watawasaliti mashabiki wao na kukubali mechi ya marudiano.

Simba kuelekea Misri Machi 28

"Kikosi kitaondoka nchini alfajiri ya tarehe 28 kuelekea Misri kwa kutumia ndege ya Egypt Air. Wachezaji wetu waliokuwa Taifa Stars wataungana na timu nchini Misri. Camara na Mukwala tayari wamewasili nchini kujiunga na wachezaji wenzao kwa ajili ya maandalizi ya safari." "Kila Mwanasimba atambue kwamba pamoja na mipango tuliyonayo lakini lazima tujipange, lazima tujiandae na hasa kama timu yenyewe inatokea Misri. Ukiangalia michuano ya Afrika ilivyo utaona kwamba Misri ndio nchi iliyoingiza timu nne kwenye robo fainali." "Tunakwenda kucheza na Al Masry tukijua tunakwenda kucheza mechi ngumu kwelikweli lakini dhamira tuliyojiwekea ni kufuzu nusu fainali." "Niwatoe hofu kwamba Uwanja wa Benjamin Mkapa umeshafanyiwa ukaguzi. Bado majibu hayajatoka lakini katika mazungumzo wanasema kuna maboresho makubwa kwenye uwanja ukilinganisha na mara ya mwisho walipofanya ukaguzi hivyo kuna nafasi kubwa ya kucheza kwenye uwanja huo. Na wote mnakumbuka kauli ya Msem...

Nigeria yataka pointi za mezani

Timu ya Taifa ya Nigeria imewaomba CAF na FIFA waweze kuwapokonya Timu ya Taifa ya Afrika Kusini alama 3 pamoja na mabao 3 waliyopata walipocheza dhidi Lesotho kwa kumjumuisha Teboho Mokoena aliyekuwa amepata Kadi za njano kwenye mechi zake 2 zilizopita, Mashabiki wa Soka, wakiongozwa na Nigeria sasa wanataka Afrika Kusini ichukuliwe hatua kwa kitendo hicho na wametaka Lesotho nao wawashtaki Afrika Kusini kwa tukio hilo.

Bodi ya Ligi kuburuzwa mahakamani

Page 1 & 2 Ni taarifa kwamba kutoka kwa mdau mmoja wa soka ambaye pia Mwachama wa Klabu ya Yanga SC kutokea mkoani Iringa ambaye ameitaka bodi ya ligi kuu ( TPLB) ndani ya siku 7 kuanzia leo kutekeleza mambo kadhaa ama sivyo ataifikisha bodi hiyo Mahakamani, Madai hayo yaliyotokana na Uamuzi usio halali wa Bodi ya ligi wa kuaihirisha Mechi namba 184 ya NBCPL tarehe 8 Machi 2025 ikiwa ni pamoja na kurejeshewa gharama alizoingia kwenda Dar kushuhudia hiyo mechi pia na Yanga kupatiwa pointi 3 na magoli matatu, Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika mkoani Iringa kinasema Demand Notice hii ilishatumwa ofisi za TFF.

Waziri Kabudi ana kwa ana Bodi ya Ligi, Yanga. Soma zaidi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la chini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria. "Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dares Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi. Msigwa pia alieleza maofisa wa Simba watashiriki katika kikao hicho. Mchezo huo, ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Mac...

Simba atutaidharau Bigman- Ahmed Ally

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema klabu hiyo haitaki kufanya makosa kuelekea mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Bigman. - Simba, inayonolewa na Kocha Fadlu Davids, itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa Alhamisi, Machi 27, katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge. - Ahmed amesema licha ya Bigman kuwa timu inayoshiriki Ligi ya Championship, jina lake linatisha, na Simba inaheshimu historia ya timu kama hizo ambazo zimekuwa zikiwasumbua katika mashindano ya ndani kwa miaka ya nyuma. - “Tunakumbuka timu za aina hii zimekuwa na historia mbaya kwetu, kwa hiyo ni lazima tufanye vizuri. Tumekuwa na wiki mbili za maandalizi kwa wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu za taifa,” alisema Ahmed. - Kwa mujibu wa Ahmed, Simba ilitumia wikiendi iliyopita kucheza mechi za mazoezi kama sehemu ya maandalizi yao kwa ajili ya mchezo huo muhimu. - “Kocha Fadlu aliona ni vyema kupata mechi ya kirafiki ndani ya wiki hii ili kupima ...

Novatus Dismas mchezaji ghali zaidi Tanzania

Kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoingia kambini March 14, 2025, Mchezaji wa Klabu ya Gotzepe ya nchini Uturuki Novatus Dismas Miroshi (22) ndiye nyota ghali zaidi katika kikosi cha timu ya taifa la Tanzania akiwa na thamani ya Pauni milioni moja (€1.0M) sawa na Shilingi ya Kitanzania Bilioni 2.8. Hii ni kwa muujibu wa Transfermarket.

Yanga yaja na ujenzi wa akademia

Klabu ya Yanga SC inaweza kuwa ya kwanza nchini kuanzisha akademia, kupitia kwa Rais wa Klabu hiyo Injinia Hersi Said ameanika ramani ya ujenzi mkubwa wa akademia hiyo itakayojengwa Kigamboni. Tayari Yanga ilishaachia ramani zake za uwanja wa Kaunda pale Jangwani ambao bado haujajengwa, lakini kwa uongozi madhubuti wa Hersi unaweza kujengwa. Ujenzi wa akademia ya klabu hiyo kubwa na kongwe Afrika mashariki, itasaidia kuzalisha wachezaji hapa nchini ambao watauzwa mataifa mengine duniani. Hongera Injinia Hersi kwa maendeleo haya ambayo yataacha historia kwa siku zijazo.

Masalanga afurahia kuitwa Taifa Stars

"Mimi nimejisikia faraja kuitwa timu ya Taifa ,Familia yangu ndio walikuwa wa Kwanza kunipa taarifa kupitia mjomba wako ,Sikuweza kuamini mpaka pale ambapo niliweza kuingia kwenye mtandao na nikaona kweli jina lako limeitwa ,Nikamshukuru Mungu" "Nimekutana na wachezaji wa level ya juu ambao wako na Uzoefu mkubwa wa kucheza mashindano makubwa kama AFCON,Nimefurah hapa kukuta kila mmoja anapambania timu ya Taifa ,Nimeshangaa Sana kuona wachezaji wako na nidhamu kubwa pia wanaishi Kwa upendo mkubwa" Hussein Masalanga ( Golikipa wa timu ya Taifa Tanzania) akizungumza baada ya kuitwa Kwa mara ya Kwanza timu ya Taifa ya Tanzania

Aziz Ki anahusika mafanikio ya Yanga Princess

Mratibu wa Yanga Princess, Kibwana Matokeo amesema kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Aziz KI amekuwa mtu muhimu kwenye matokeo ya timu hiyo akiwapa sapoti wachezaji wa kike. Aziz KI kwenye mechi mbalimbali za Ligi ya Wanawake amekuwa akionekana uwanjani, Yanga Princess inapocheza ikiwa mchezo wa Dabi dhidi ya Simba Queens. Akizungumza na Mwanaspoti, Matokeo alisema nyota huyo raia wa Burkina Faso amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho akiwapa hamasa wachezaji wa kike kwenye mechi mbalimbali.