Yanga yaingia mkataba na Kamisheni ya Utalii Zanzibar

Kamisheni ya Utalii Zanzibar imeingia rasmi katikaushirikiano na klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga SC) kwa kusaini mkataba wa kutangaza vivutio vya Zanzibar kupitia kauli mbiu ya “Visit Zanzibar.”

Mkataba huo umesainiwa tarehe 28 Machi 2025, na KatibuMtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ndugu Arif Abbas pamoja na Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said, mbele ya mgeni rasmi Mheshimiwa Mudrik R. Soraga, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, ambaye alishuhudiatukio hilo muhimu.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii, Arif Abbasalieleza kuwa kupitia kampeni ya “Visit Zanzibar” kwenye jezi za Yanga, Zanzibar itanufaika kwa kufikia soko la kutangaza utalii wa ndani “Domestic Tourism”, Utalii wakikanda na bara zima la Afrika kutokana na umaarufu wa timuhiyo na wachezaji wake kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

Kwa upande wake, Eng. Hersi Said alieleza furaha ya klabuyake kushirikiana na Kamisheni ya Utalii Zanzibar. “Kwa msimu mzima wa 2025/2026, nembo ya Visit Zanzibaritawekwa kwenye jezi rasmi za Yanga kwa mashindano yote. Pia tumejipanga kutoa elimu na hamasa kwa Watanzaniakutembelea vivutio vya nyumbani. Hakuna sababu ya kwendaIbiza au Dubai ilhali tunayo Zanzibar,” alisema.