KOCHA wa Yanga, Hamdi Miloud, amesema anahitaji kuingia na kikosi cha ushindani katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tabora United, akisisitiza umuhimu wa kupata ushindi.
-
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumatano, Aprili 2, kwenye Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, Tabora. Yanga inakwenda katika mechi hiyo ikiwa na morali baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa kuiondoa Songea United.
-
Kocha Hamdi amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma katika mchezo dhidi ya Songea United na kueleza kuwa maandalizi ya mchezo ujao yanaendelea kwa nguvu.
-
Ameongeza wanatambua changamoto ya kucheza ugenini, hasa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza walipokutana na Tabora United, lakini wanajipanga kulipa kisasi.