Klabu ya Pamba Jiji kutoka Jijini Mwanza imeibuka na ushindi Wa Bao 1-0 Dhidi ya klabu ya Mashujaa Fc ya Mkoani Kigoma katika mchezo Wa hatua ya 16 Bora ya Michuano ya CRDB Federation Cup mchezo ambao umepigwa majira ya Saa 10:00 Jioni katika dimba la Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.
Bao la Pamba Jiji limefungwa na nyota wao Allan Mukeya na kuifanya Pamba Jiji kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo.