WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wametangulia kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CRDB Cup baada ya kuilaza Bigman- FC mabao 2-1 uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo wa michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mzambia, Joshua Mutale dakika ya 16 na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 31, wakati bao pekee la Big Man FC limefungwa na Joseph Henock dakika ya 45.