Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC Murtaza Mangungu amesema wao hawakuitwa na Waziri Kabudi kwa ajili ya sakata la mechi ya dabi dhidi ya Yanga isipokuwa waliitwa kujadili maendeleo ya soka la Tanzania.
Amedai Simba ndio timu pekee inayowakilisha nchi kimataifa hivyo ni wajibu kushirikishwa kwenye mambo makubwa.
"Kikao chetu sisi kimejadili maendeleo ya mpira hakijajadili walichojadiana na wenzetu, tungejadili mechi yetu tungeitwa kwa pamoja ila mamlaka si ilishasema mechi yetu itapangiwa tarehe nyingine."
"Sisi tumejadili maendeleo ya soka Tanzania, Kikao chetu sisi hakihusiani na chao."
Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba.