Waziri Kabudi ana kwa ana Bodi ya Ligi, Yanga. Soma zaidi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi amepanga kukutana viongozi wa Shirikisho la Soka la chini (TFF), Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) na Klabu ya Yanga ili kutatua mgogoro unaoendelea kuhusu kusogezwa mbele kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu Machi 24, 2025, kikao hicho kitafanyika jini Dar es Salaam, Alhamisi na maofisa kutoka Yanga, Simba, TFF na Bodi ya Ligi Kuu wamejulishwa na watahudhuria.
"Ni kweli tutakutana na Waziri Kabudi kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo kusogezwa mbele kwa mchezo wetu dhidi ya Simba. Tumepokea barua na tutahudhuria," alisema afisa mmoja wa Yanga aliyeomba kutotajwa kwa jina.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alithibitisha kikao hicho kitafanyika jijini Dares Salaam kikiongozwa na Waziri Kabudi. Msigwa pia alieleza maofisa wa Simba watashiriki katika kikao hicho.

Mchezo huo, ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliahirishwa baada ya Simba kudai makomandoo wa Yanga waliwakatalia kuingia uwanjani kwa ajili ya mazoezi yao ya kabla ya mchezo.