Bodi ya Usuluhishi wa Kesi za Kimchezo ya CAS imethibitisha kupokea barua ya Yanga ambapo Walalamikiwa ni TFF, BODI na SIMBA.
Walalamikiwa wamepewa siku 10 baada ya kupokea taarifa rasmi kutoka CAS kuanza kuandaa utetezi wao wakati mchakato wa kesi unaanza rasmi kusikilizwa kwa nyaraka yenye kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298.