Rais wa Klabu ya Rayon Sports ya Nchini Rwanda Twagirayezu Thaddee amethibitisha kuwa Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa ipo tayari kucheza nao kwenye mchezo wa kirafaiki katika uwanja mpya wa Amahoro kujiandaa na Msimu mpya wa Mashindano wa 2025/26.
Pia kwasasa Klabu ya Rayon Sports ambao ni kinara wa ligi kuu ya Rwanda na ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu mbele ya APR.
Rayon Sports ipo chini ya Kocha wa zamani wa klab ya Simba Raia wa Brazil Oliveira Roberto ' @robertinho7.coach
Kwa mujibu wa moja ya Chapisho la Michezo kutoka Nchini Rwanda lilianduka kuwa Uongozi wa klab ya Rayon Sports licha ya Raisi wa klab yao kuwa na Ukaribu mzuri na Raisi wa klab ya Young Africans Hersi Said pia klab ya Yanga ni miongoni mwa Vilabu pendwa kwasasa Nchini Rwanda na Afrika.
Young Africans ndio Vinara wa ligi kuu ya Tanzania na ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu huu.