Timu ya Taifa ya Nigeria imewaomba CAF na FIFA waweze kuwapokonya Timu ya Taifa ya Afrika Kusini alama 3 pamoja na mabao 3 waliyopata walipocheza dhidi Lesotho kwa kumjumuisha Teboho Mokoena aliyekuwa amepata Kadi za njano kwenye mechi zake 2 zilizopita,
Mashabiki wa Soka, wakiongozwa na Nigeria sasa wanataka Afrika Kusini ichukuliwe hatua kwa kitendo hicho na wametaka Lesotho nao wawashtaki Afrika Kusini kwa tukio hilo.