Yanga yaja na ujenzi wa akademia

Klabu ya Yanga SC inaweza kuwa ya kwanza nchini kuanzisha akademia, kupitia kwa Rais wa Klabu hiyo Injinia Hersi Said ameanika ramani ya ujenzi mkubwa wa akademia hiyo itakayojengwa Kigamboni.

Tayari Yanga ilishaachia ramani zake za uwanja wa Kaunda pale Jangwani ambao bado haujajengwa, lakini kwa uongozi madhubuti wa Hersi unaweza kujengwa.

Ujenzi wa akademia ya klabu hiyo kubwa na kongwe Afrika mashariki, itasaidia kuzalisha wachezaji hapa nchini ambao watauzwa mataifa mengine duniani.

Hongera Injinia Hersi kwa maendeleo haya ambayo yataacha historia kwa siku zijazo.