Mbeya City yamtambulisha Malale Hamsini

Timu ya Mbeya City (Wanakoma Kumwanya) ya jijini Mbeya imemtambulisha Malale Hamsini kuwa kocha wao mpya, akichukua nafasi ya Salum Mayanga aliyekwenda kuifundisha Mashufaa FC.

Kazi kubwa inayomkabili kocha Malale Hamsini ni kuhakikisha Mbeya City inarejea Ligi Kuu msimu ujao.

Kwa sasa, Mbeya City inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ikiwa na alama 55 baada ya michezo 25, ikizidiwa alama tano na Mtibwa Sugar, huku zikiwa zimesalia mechi tano pekee.

Malale Hamsini, mzawa wa Zanzibar, ana uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania Bara, kwani amewahi kufundisha zaidi ya timu tatu za Ligi Kuu, huku timu yake ya mwisho ikiwa JKT Tanzania.