Mabingwa watetezi wa kombe la CRDB Cup, Yanga SC jioni ya leo wameifunga Songea United ya mkoani Ruvuma mabao 2-0 uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Duke Abuye dakika ya 21 na Jonathan Ikangalombo dakika ya 54 yametosha kuipeleka hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo bingwa wake anakwenda kushiriki kombe la Shirikisho barani Afrika.