KLABU ya Young Africans imeendelea na Msimamo wa kutocheza Mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Simba mchezo ambao awali ulipangwa kuchezwa Machi 8 mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa Young Africans Ali Kamwe wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Visiwani Zanzibar mara baada ya kumalizika Kwa utiaji wa saini wa makubaliano baina ya Young Africans na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar, kuhusu kuitangaza Zanzibar kupitia “Visit Zanzibar”.