Saudi Arabia wametangaza Mwandamo wa Mwezi jamba ambalo linaashiria kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kesho Jumapili ni Eid Al Fitr.
Kwa upande wa Tanzania tayari Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr inatarajiwa kuwa Machi 31 au Aprili mosi, kulingana na mwandamo wa mwezi.
Sherehe za kitaifa zitafanyika jijini Dar es Salaam ambapo Swala ya Eid itaambatana na Baraza la Eid litakalofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere saa 9 Alasiri. Mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.