Walionunua tiketi za Constantine kuiona Al Masr - Simba SC

Klabu ya Simba imetangaza kuwa mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi za mechi yao dhidi ya Constantine watazitumia kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Masry ya Misri.

Hayo yamebainishwa na Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally Machi 26, 2025.

"Wale wote ambao walinunua tiketi dhidi ya Constantine watatumia tiketi zao kwenye mchezo dhidi ya Al Masry."

Uamuzi huo umekuja baada ya CAF kuiadhibu Simba kwa kucheza mechi moja bila mashabiki na faini ya dola 40,000 kufuatia vurugu zilizoibuka kwenye mechi yao dhidi ya CS Sfaxien ya Algeria mnamo Desemba 15, 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.