Winga wa KenGold Bernard Morrison amesema licha ya kurejea mazoezini na wenzake lakini bado hajawa fiti kuchèza mechi akiomba muda zaidi kuwa sawa, huku akilia kuikosa Ligi Kuu.
Nyota huyo raia wa Ghana alitambilishwa kikosini humo dirisha dogo akiwa huru, ambapo hajacheza mechi yoyote kati ya saba iliyochezwa na timu hiyo kufuatia majeraha ya paja yaliyokuwa yanamsumbua.
Kutokana na hali hiyo, benchi la ufundi lilimpa program maalumu ya kujifua kivyake ambapo kwa sasa tayari ameungana na wenzake kujiwinda pamoja kwa ajili ya mwendelezo wa Ligi inayotarajia kuendelea April 3.
Nyota huyo akiwa Yanga SC msimu wa 2019/20 alicheza mechi 13 akifunga mabao manne na asisti tatu, ambapo msimu uliofuata alijiunga na Simba SC akiifungia mabao manne na kuhusika mengine saba kati ya mechi 24.