Mratibu wa Yanga Princess, Kibwana Matokeo amesema kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Aziz KI amekuwa mtu muhimu kwenye matokeo ya timu hiyo akiwapa sapoti wachezaji wa kike.
Aziz KI kwenye mechi mbalimbali za Ligi ya Wanawake amekuwa akionekana uwanjani, Yanga
Princess inapocheza ikiwa mchezo wa Dabi dhidi ya Simba Queens.
Akizungumza na Mwanaspoti, Matokeo alisema nyota huyo raia wa Burkina Faso amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho akiwapa hamasa wachezaji wa kike kwenye mechi mbalimbali.