Kama mambo yataenda kama yalivyo, Azam FC ina mpango wa kumtema kipa wake Mohamed Mustafa raia wa Sudan sababu ikitajwa ni kufanya makosa mengi akiwa golini, hivyo umeanza mchakato wa kumsaka mbadala wake atakayewasaidia msimu ujao.
Chanzo cha ndani kutoka Azam FC kinasema tayari uongozi wa timu hiyo umcanza mazungumzo na kipa namba moja wa As Vita ya DR. Congo. Farid Ouedraogo na kama dili likitiki basi Mustapha atapewa mkono wa kwaheri