Klabu ya Zamalek ya Nchini Misri imepinga uamuzi wa Chama cha vilabu Nchini humo kuhusu kutenguliwa kwa adhabu dhidi ya Al Ahly ikiitaja hatua hiyo kuwa ni kama udhalimu kwenye mpira.
Haya yanajiri baada ya Chama cha vilabu kutangaza kuwa Al Ahly hawatakatwa pointi tatu mwishoni mwa msimu ingawa Zamalek watapatiwa pointi tatu baada ya Al Ahly kugomea kupeleka timu uwanjani kwenye mchezo baina ya timu hizo.
Hata hivyo Zamalek imepinga vikali hatua hiyo kwa kile ilichodai ni kutojali maslahi ya mashabiki wa thamani wa timu hiyo na haitaridhia kudhulumiwa haki yoyote huku wakitaka Ahly apokwe alama kama awali na wao kupewa ushindi huo kikanuni kama kawaida.