Kagera Sugar ya Juma Kaseja imetinga robo fainali ya Kombe la CRDB kwa kuwaondoa Tabora United kwa mikwaju ya penati 3-5 baada ya sare ya 1-1.
Katika dakika 90 za mchezo huo, Tabora United ilitangulia kwa bao la beki wake Mkongo, Andy Bikoko dakika ya tatu, kabla ya kiungo mzawa, Joseph Mahundi kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 28.
Kagera Sugar inaungana na Singida Black Stars, JKT Tanzania, Mbeya City, Stand Utd na Simba SC ambazo zimeshatinga robo fainali ya Kombe la CRDB BANK.
Kagera Sugar imebebwa na uzoefu wa wachezaji wake waliokuwa nao, Tabora United licha ya kuwa na wachezaji bora lakini imetupwa nje.
Kipa Ramadhan Chalamanda ni shujaa wa mchezo kwa kuisaidia timu yake kutinga robo fainali kwa kuzuia mchomo wa penalti.