Simba, Al Masr kucheza kwa Mkapa

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kutumika kwa mechi zote za robo fainali au nusu fainali kwa klabu ya Simba.

Awali CAF ilitangaza kuufungia uwanja huo baada ya kutoridhishwa na ukaguzi uliofanywa na wakaguzi wake, kwa maana hiyo sasa Simba itarudiana na Al Masr katika uwanja huo.

Tayari Simba ilijiandaa kusafiri Rwanda ama Uganda kwa ajili ya kutumia kama uwanja wa nyumbani baada ya kuzuiwa kwa Mkapa.