"Kikosi kitaondoka nchini alfajiri ya tarehe 28 kuelekea Misri kwa kutumia ndege ya Egypt Air. Wachezaji wetu waliokuwa Taifa Stars wataungana na timu nchini Misri. Camara na Mukwala tayari wamewasili nchini kujiunga na wachezaji wenzao kwa ajili ya maandalizi ya safari."
"Kila Mwanasimba atambue kwamba pamoja na mipango tuliyonayo lakini lazima tujipange, lazima tujiandae na hasa kama timu yenyewe inatokea Misri. Ukiangalia michuano ya Afrika ilivyo utaona kwamba Misri ndio nchi iliyoingiza timu nne kwenye robo fainali."
"Tunakwenda kucheza na Al Masry tukijua tunakwenda kucheza mechi ngumu kwelikweli lakini dhamira tuliyojiwekea ni kufuzu nusu fainali."
"Niwatoe hofu kwamba Uwanja wa Benjamin Mkapa umeshafanyiwa ukaguzi. Bado majibu hayajatoka lakini katika mazungumzo wanasema kuna maboresho makubwa kwenye uwanja ukilinganisha na mara ya mwisho walipofanya ukaguzi hivyo kuna nafasi kubwa ya kucheza kwenye uwanja huo. Na wote mnakumbuka kauli ya Msemaji Mkuu wa Serikali alivyosema kwamba uwanja upo tayari. Hatuna muda wa kusubiri tunafanya maandalizi."- Ahmed Ally Semaji la CAF