Msemaji wa klabu ya Yanga SC Ally Kamwe amesema mechi yao ya Jumatano dhidi ya Tabora United itakayofanyika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi itakuwa nyepesi na wala si ngumu ila kuna watu wanataka kuiona ngumu.
"Kiukweli kabisa wa mpira Jumatano sisi Yanga SC hatuna mechi ngumu hapa Tabora ila wapo watu wachache kwasababu zao sijui za kisiasa wanataka kukaa mbele wazungumze wasikike na waonekane hao ndio wanawaaminisha watu kuwa jumatano Ally Hassan Mwinyi kutakuwa na mchezo mgumu kwelikweli huo ni uongo."
.
"Sisi Yanga tuna muheshimu sana Rais Samia ila huyu mtu wake aliyemtuma huku Tabora anatuchokonoa anatutafuta la rohoni sisi Yanga, Kiheshima tunamuomba radhi kwanza aliyemtuma halafu Yanga tunashuhulika nae, tumwambie mkuu wa mkoa Paul Chacha jumamosi atachacha kweli."
.
Amesema Ally Kamwe Meneja Habari wa Klabu ya Yanga SC.