Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2025

Lidya Okoth amalizana na Yanga Princess

Klabu ya Yanga Princess imetambulisha kiungo mshambuliaji Lidya Akoth raia wa Kenya kuwa mchezaji wao kutokea klabu ya Kenya Police Bullets. Msimu uliopita katika raundi ya pili Lidya aliitumikia klabu ya Yanga Princess kwa mkopo wa miezi sita kutokea klabu ya Kenya Police Bullets. Sasa ni rasmi Lidya Akoth ni mali ya Yanga Princess kwa mkataba wa miaka miwili. Attacking mid ya Yanga Princess ; 1. Lidya Akoth 2. Precious Christopher 3. Adebis Ameerat 4. Riticia Nabbosa (ambaye pia anaweza kutumika kama namba 6).

Aucho aitwa The Cranes

Kiungo mkabaji mpya wa Singida Black Stars, Khalid Aucho ameitwa kwa mara ya kwanza na timu ya taifa ya Uganda The Cranes tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea kwa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC. Aucho aliachana na Yanga baada ya kushindwana katika suala la kuongeza mkataba, hivyo kiroho safi Yanga walimpa thank you, lakini mabosi wa Singida Black Stars walipita naye.

Simba yatambulisha jezi mpya

KLABU ya Simba jana usiku imetambulisha rasmi jezi zake za msimu mpya chini ya mzabuni mpya wa vifaa vyake bus michezo Kampuni ya Jay Rutty.  Nyekundu ni jezi za nyumbani. Nyeupe ni jezi ya ugenini. Buluu ni jezi ya ziada ‘third kit’.

Clatous Chama akamilisha usajili Singida Black Stars

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga, Mzambia Clatous Chama, amekamilisha usajili wa kujiunga na wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, Singida Black Stars kwa kandarasi ya mwaka mmoja. Tayari Chama alishaanza mazoezi na timu hiyo na usajili wake ni mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo Miguel Gamondi raia wa Argentina. Ikumbukwe Chama na Gamondi walikutana Yanga msimu uliopita, Chama pia anaungana na Khalid Aucho na Nickson Kibabage. Kila la kheri nyota hao ndani ya Singida Black Stars.

Haji Manara akanusha kurejea Simba

Mkurugenzi Mtendaji wa Manara TV Haji Manara amekanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni kwamba anatarajia kurejea kufanya kazi katika klabu ya Simba SC. Akizungumza na Manara Tv, Manara amesema, "Nimeona na mimi nimetumiwa mitandaoni kwamba naenda tena kufanya kazi Simba, na watu wengi mmeniuliza. Jawabu langu ni Uongo, sina mpango huo kwa sasa mimi naendelea kuwa mshabiki na mwanachama wa Yanga ingawa niko mbali na mambo haya kwa sasa lakini bado nafuatilia kwa karibu kila kinachoendelea ndani ya klabu yangu, nalipa ada za uanachama," alisema Manara na kuongeza kuwa; "Ni kweli nliwahi kufanya kazi Simba lakini siwezi kurudi na moyo wangu uko Yanga, hata kama kwa sasa sifanyi kazi Yanga lakini moyo wangu uko Yanga na niwaombe wanachama na washabiki wa Yanga wapuuze hadithi za mitandaoni ambazo wakati mwingine zina lengo ovu, zina lengo baya dhidi yangu na hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba ambao mimi nagombea nafasi ya Udiwani Kari...

Jesus Moloko atimkia Rwanda

Winga wa zamani wa Yanga SC,  Jesus Moloko amejiunga na Klabu ya AS Kigali kwa mkataba wa Mwaka mmoja. Moloko alikuwa kwenye kiwango bora alipokuwa katika klabu ya Yanga SC akiwa sambamba na mshambuliaji Fiston Mayele ambaye sasa yupo Pyramids. Akiwa Yanga, Moloko aliisaidia kutwaa ubingwa wa bara misimu mitatu aliyokaa.

Yanga Princess yaachana na Sportpesa

Timu ya Yanga Princess haitaitangaza tena kampuni ya kubashiri SportPesa. Hii ni kutokana na uamuzi wa timu hiyo kutafuta mdhamini wake wa kujitegemea, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo udhamini wa timu ya wanaume ulihusisha pia timu ya wanawake. Kuanzia sasa, wachezaji watakaotambulishwa hawatakuwa na tangazo lolote la SportPesa—iwe kwenye jezi za mazoezi, jezi za mechi, au mavazi yao mengine yote. Yanga Princess sasa ipo kwenye mchakato wa kutafuta mdhamini mpya, na pia inakaribisha makampuni mbalimbali kujitangaza kupitia timu ya wanawake ya Yanga Princess. Huu ni wakati wa mapinduzi—tuanze kuzipa thamani timu zetu za wanawake kwa kujitegemea katika udhamini, ili kuongeza hadhi yao na kupunguza mzigo wa kifedha ndani ya vilabu vyetu.

Beki mpya Simba kuvunja mkataba..

Beki wa Kushoto wa Simba SC Antony Mlingo amegoma kuendelea na shughuli yoyote katika kikosi cha Simba mpaka atakapolipwa pesa zake zote alizoahidiwa. Chanzo chetu cha Kuaminika kimetutaarifu kuwa Mlingo yupo mbioni kuvunja mkataba na wekundu wa Msimbazi Simba. Mligo anaweza kuachana na Simba kwa sababu ya wakala wake ambaye haelewani na Simba, wakala wa Mligo ndiye huyo huyo wakala wa Mohamed Hussein Tshabalala ambaye alidhindwana na Simba na kuamua kuondoka. Wakala huyo ni Carlos Mastermind.

Kipa Azam FC atimkia Al Hilal Omduman

#DEAL_DONE ✅✅ Golikipa wa timu ya taifa wha Sudan 🇸🇩,  Mohamed Mustafa amejiunga na Klabu ya Al Hilal ya Sudan 🇸🇩  kwa Mkataba wa Miaka mitatu mpaka 2028. . Mustafa amejiunga na Al Hilal baada ya kuachana na klabu ya Azam FC aliyokuwa akiitumikia.

Taifa Stars kuingia kambini Septemba 2

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Hemed Morocco ametangaza kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini Septemba 2, 2025 kwa ajili ya kujiandaa na michezo miwili ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Congo Brazzaville na Niger huku nahodha Mbwana Ally Samatta akiwa miongoni mwa walioitwa.

Haji Manara kumrithi Ahmed Ally Simba SC

Taarifa zilizotufikia ni kwamba Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally anakuwa Mkurugenzi wa mashabiki wa klabu ya Simba SC na aliyekuwa msemaji wa Yanga SC, Haji Manara anarejea kuwa Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC. Ahmed Ally tayari ameshaanza majukumu yake ya Ukurugenzi wa mashabiki na jana alikuwa Mafinga kukamilisha uzinduzi wa Simba Day, muda si mrefu Haji Manara anakwenda kutambulishwa kurejea kwenye nafasi yake. Ikumbukwe Manara alipokuwa msemaji wa Simba, ikifanikiwa kushinda makombe yote ya Tanzania bara katika misimu minne mfululizo. KARIBU Msimbazi Haji Manara

Timu itakayokwepa kupeleka timu uwanjani kukutana na hiki

Kanuni ya 31, Kutofika uwanjani:- Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika kwa TPLB au mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu ya kupoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu. 31 (1.2). Lakini pia timu kutozwa faini isiyopungua shilingi milioni hamsini (50,000,000/-) ambapo 50% ya faini itachukuliwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na 50% italipwa kwa timu. 31 (4.1). Timu Kupokwa alama 3 katika msimamo wa Ligi pamoja na Mwenyekiti au Rais wa Klabu kufungiwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.

Mlandege FC yasajili mchezaji wa Ufaransa

klabu ya Mlandege FC imekamilisha usajili wa kiungo nyota Enzo Claude raia wa Ufaransa  mwenye uwezo wa kucheza namba 8 ama 10. Mlandege wamefanya kufuru ya fedha na usajili! 

Morocco mabingwa CHAN

TIMU ya taifa Morocco imefanikitwa kutwaa Kombe la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar usiku huu Uwanja wa Moi International Sports Centre, Kasarani, Nairobi nchini Kenya. Ilikuwa mechi ya funga nikufunge, kabla ya mshambuliaji wa mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, RS Berkane – Oussama Lamlioui kufunga bao la ushindi dakika ya 82. Hilo lilikuwa bao lake la pili kwa Lamlioui kwenye mchezo huo kufuatia kufunga lingine dakika ya 44 ambalo lilielekea kuwa la ushindi – kabla ya winga wa COSFAP Antananarivo, Toky Niaina Rakotondraibe kuisawazishia Madagascar dakika ya 68. Madagascar ndio waliouanza vizuri mchezo huo na kupata bao la kuongoza kupita kwa mshambuliaji wa Fosa Juniors FC, Felicite Manohantsoa dakika ya tisa, kabla ya winga wa Renaissance de Berkane, Youssef Mehri kuisawazishia Morocco dakika ya 27. Hilo linakuwa taji la tatu la CHAN kwa Morocco baada ya awali kulibeba katika mwaka 2018 na 2020, hivyo kuweka rekodi ya kuwa ti...

Nyota Yanga aikacha nchi yake ya asili

Mshambuliaji mpya wa Young Africans SC Celestine Ecua ameamua kuichagua Nchi ya Chad ambayo ni nchi yake ya pili kuitumikia kwenye timu ya taifa akiikacha Ivory Coast,  Sababu kubwa ya Ecua kuichagua Chad  ili apate nafasi ya kucheza mara Kwa mara sababu kikosi cha Ivory Coast kimesheheni mastaa wanaokipiga Ulaya .

Mbosso kupamba Simba Day

Msanii wa muziki wa kizaxi kipya aliyewahi kuwa memba wa lebo za Yamoto Band na WCB, Mbwana Yusuf Kilungi "Mbosso" atapamba tamasha kubwa la klabu ya Simba la Simba Day siku ya Septemba 10 mwaka huu katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Klabu ya Simba imeweka wazi hii leo kupitia msemaji wake Ahmed Ally ambapo Mbosso atakuwa jukwaa kuu akiwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo.

Pipino kaota mbawa Simba

Dili la kiungo Ahmed Pipino kujiunga na klabu ya Simba SC limekufa ramsi baada ya Magnet Academy ambao wanammiliki mchezaji huyo kuhitaji kiasi cha pesa cha Tshs 200M ili auzwe kutoka KMC FC Awali klabu ya KMC ilitaja kiasi cha Tshs 150M ili imuachie kiungo huyo huku Magnet Academy wakihimiza kuwa wao ndio wanamamlaka zaidi na kiungo huyo na thamani yake ni hiyo waliyoitaja na mpaka sasa Simba SC wamesitisha mauzo yake wakiamini kiungo huyo ana thamani ya Tshs 150M na ikiwa watatoa Tshs 200M ndio Magnet Academy watamuachia kiungo huyo.

AHADI ZA DKT SAMIA AKIINGIA IKULU

Mgombea wa Urais Kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2025 ametoa ahadi zifuatazo katika siku zake 100 za kwanza akiwa madarakani; ✅ Marufuku kuzuia maiti hospitalini ✅ Bima ya Afya kwa Wazee, Watoto, Walemavu   ✅ Wagonjwa wa saratani, sukari, figo kugharamiwa   ✅ Wahudumu 5,000 wa afya kuajiriwa   ✅ Walimu wapya 7,000 kuajiriwa    ✅ Bilioni 200 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo   ✅ Kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya   ✅ Mawaziri, wakuu wa mikoa kuwajibika kwa wananchi   ✅ Kurasmisha sekta isiyo rasmi   ✅ Kuanzisha Gridi ya Taifa ya Maji

Bernard Morrison afunika usajili Bangladeshi

Klabu ya Mohammedan Sporting Club ya nchini Bangladesh Premier League. amekamilisha usajili wa mchezaji Bernard Morrison.  Anatajwa kama nyota mkubwa zaidi kuwahi kusajiliwa katika historia ya ligi hiyo.. Ikumbukwe Morrison aliwahi kuzichezea Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Yanga na Simba za Tanzania na DC Motema Pembe ya DR Congo 

Yanga Princess yatambulisha kocha mpya

Klabu ya Yanga Princess imemtambulisha kocha wake mpya wa utimamu wa mwili/viungo (fitness coach), Brenda Chaora raia wa Zimbabwe. Brenda kabla ya kujiunga na Yanga Princess aliwahi kuwa kocha wa Fitness wa Simba Queens (timu ambayo iliyomtambulisha katika soka la Tanzania),kisha baadae akajiunga na Fountain Gate Princess na sasa amejiunga na Wananchi. Ubora wake,taaluma,Uzoefu na Elimu yake ndio vitu bora zaidi na vya pekee vinavyotenga daraja lake na baadhi ya makocha wengi wa fitness hapa nchini.

Senegal yakamata nafasi ya tatu CHAN

TIMU ya Senegal imefanikisha kumaliza nafasi ya tatu katika Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kufuatia ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Sudan baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda leo. Winga wa Al-Merrikh SC, Muhamed Tia Asad alianza kuifungia Sudan dakika ya sita, kabla ya beki wa Kati wa FC Gorée, Seyni Ndiaye kuisawazishia Senegal dakika ya 16. Waliofunga penalti za Senegal ni Joseph Layousse, Issa Kane, Vieux Cissé na Libasse Guèye, wakati waliofunga za Sudan ni Mohamed Ahmed Saeed na Ahmed Tabanja pekee, huku Walieldin Khdir akipiga nje na ya Musab Makeen ikiokolewa na Marc Diouf. Fainali ya CHAN 2024 itafuatia kesho kuanzia Saa 12:00 jioni baina ya Madagascar na Morocco Uwanja wa Moi International Sports Centre, Nairobi, Kenya.

Yanga haitanii, yaichapa Tabora United 4-0 kirafiki

TIMU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Gymkhana Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua na washambuliaji Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo na Ange Celestin Ecua aliyesajiliwa dirisha hili kutoka Zoman FC ya kwao, Ivory Coast. Huo unakuwa mchezo wa nne wa kujipima nguvu kwa Yanga katika maandalizi ya msimu mpya na kuendeleza rekodi ya ushindi. Mechi tatu za awali ilishinda 3-1 dhidi ya Rayon Sports Jijini Kigali nchini Rwanda, 2-1 dhidi ya Fountain Gate na 4-0 dhidi ya wadogo zao, U20 zote Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Msimu Yanga ipo chini ya Benchi jipya kabisa la Ufundi Yanga chini ya Kocha Mkuu, Mfaransa Romain Folz na Msaidizi wake, Mspaniola Alejandro Manu Rodríguez Lázaro na Kocha wa Makipa, Majdi Mnasria. Wengine ni Mtaalamu wa Viungo (Physiotherapist), Youssef Ammar wote kutoka Tunisia, Kocha wa Phy...

Tshabalala aripoti mazoezini Yanga

BEKI Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ leo ameripoti katika klabu yake mpya, Yanga SC kuanza maandalizi ya msimu mpya na kwa ujumla maisha mapya Uyangani baada ya kuachana na Simba SC aliyoichezea kwa muda mrefu.

Kila kombe litatua Simba- Sowah

Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Jonathan Sowah raia wa Ghana, amesema leo kwamba kila kombe ambalo Simba SC itashiriki lazima litue Msimhazi kutokana na maandalizi waliyonayo kwa sasa. Sowah ameyasema baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam na timu yake ya Simba iliyokuwa kambini nchini Misri. “Mashabiki wa Simba wasijali hata kama naikosa Ngao ya Jamii ila tutakutana nao kwenye Ligi hilo ndilo jambo la msingi, ndoto yetu ni kuleta kila kombe Msimbazi” Amesema Jonathan Sowah, Mshambuliaji wa Simba SC

Simba yamsajili beki na kumtoa kwa mkopo

Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa beki wa kati Vedastus Masinde (19) kutoka TMA inayoshiriki Ligi daraja la kwanza Tanzania Simba SC imempeleka Vedastus Masinde kujiunga na JKT Tanzania kuelekea msimu ujao ili kuboresha kiwango chake ikiwa ni makubaliano ya uhamisho wa Yakoub Suleiman na Wilson Nangu

Simba Day ni Simba SC vs Gor Mahia

KLABU ya Simba itacheza na vigogo wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki kwenye tamasha la Simba Day Septemba 10 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

JKT Tanzania yakubali yaishe kwa Simba kuhusu Nangu na Yakoub

KLABU ya JKT Tanzania imeachana na Wachezaji wake wawili tegemeo wa safu ya ulinzi, kipa Yacoub Suleiman Ali (25) na beki Wilson Edwin Nangu (23) ambao wote wapo mbioni kujiunga na Simba SC. Wawili hao wamekuwa wakitajwa katika taarifa za chanzo mbalimbali kuwa katika mazungumzo na Simba SC na taarifa hizi za JKT kuachana nao mara tu baada ya kumaliza majukumu hao katika timu ya taifa zinaashiria ukweli. Yakoub amedaka mechi zote tano za timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Katika Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ikitolewa katika hatua ya Robo Fainali akiruhusu mabao mawili tu. Nangu bado ni beki wa benchi Taifa Stars ambaye kwa kipaji na juhudi zake anatabiriwa makubwa siku za usoni. Yakoub amedumu kwa misimu miwili tu JKT Tanzania tangu awasili kutoka JKU ya Zanzibar, wakati Nangu ameichezea timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa msimu mmoja tu akitokea TMA Stars ya Arusha.

#TupoNaMama: Mkinichagua tena nitapiga marufuku hospitali kuzuiya maiti

Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema endapo atapata ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa mara nyingine atapiga marufuku Hospitali kuzuia miili ya Marehemu kuchukuliwa na Ndugu zao. Dkt. Samia amesema hayo kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho viwanja vya Tanganyika packers Kawe, Dar es salaam.

Afisa Habari Mlandege abwaga manyanga

Afisa Habari wa Klabu ya Mlandege, Ally Mohamed amejiuzulu nafasi yake kuanzia leo Agosti 21, 2025.  Inatajwa kuwa Ally anatarajiwa kujiunga na klabu nyengine ya Ligi Kuu Zanzibar mwanzoni mwa msimu huu mpya.  Hatua hii inakuja, zikiwa zimesalia siku chache kuelekea michuano ya kimataifa ambapo Mlandege ipo katika maandalizi ya michuano hiyo. Karibu miaka 2 imepita toka Ally alipojiunga na Mlandege kama Afisa habari wa klabu hiyo.

Popat wa Azam FC abeba tuzo

CEO wa Azam FC Abdulkarim Amin Popat ameshinda tuzo ya Visionary Award kama kiongozi bora wa mwaka kwenye michezo, tuzo hizo zimetolewa na THE 200 CEO's BUSINESS FORUM zikimtambua POPAT kama mchapakazi kwenye sekta ya michezo na uongozi bora! 

Yanga Princess ni nyumbani nimeamua kurudi- Precious

KIUNGO wa kimataifa kutoka Nigeria, Precious Christopher, amesema kurejea kwake Yanga Princess ni kama kurudi nyumbani baada ya kutambulishwa rasmi na klabu hiyo jana jijini Dar es Salaam. - Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Precious aliandika: “Nyumbani!! Nyumbani!! Nyumbani!! Aya ndugu zangu nimesikiliza na nimerudi nyumban, Mimi siku zote ni Mwananchi," - Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 aliwahi kuichezea Yanga Princess kabla ya kusajiliwa na Simba Queens msimu uliopita, ambako alisaini mkataba wa miaka miwili na kuonesha kiwango bora akiwa kiungo mkabaji mwenye nguvu na pasi sahihi. -  Msimu uliopita alifunga mabao matatu na kutoa pasi ya bao moja katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL). - Mbali na Precious, Yanga Princess pia wamemtambulisha kiungo mwingine mpya, Ritticia Nabossa kutoka Uganda, ambaye awali alicheza Fountain Gate Princess kisha kujiunga na Simba Queens na Wincate Kaari. - Nabossa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa timu ya taifa ya wanawak...

Betika kudhamini kombe la Kagame

KAMPUNI ya michezo ya Kubahatisha, Betika imedhamini michuano ya Klabu za Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Cup 2025 inayotarajiwa kuanza Septemba 2 hadi 15 Jijini Dar es Salaam kwa dau la Shilingi Milioni 42 za Kenya, Zaidi ya Shilingi Milioni 813.9 za Tanzania. Mkataba baina ya Betika na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) umesainiwa leo Jijini Nairobi nchini Kenya ukishuhudiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Wallace John Karia ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CECAFA, Mama Doris Petra. Mtendaji Mkuu wa Betika, Mutua Mutava amesema katika hafla hiyo kwamba wamedhamini michuano hiyo kutokana na Imani yao katika maendeleo ya soka ya ukanda wa CECAFA. Katika droo iliyopangwa leo hoteli ya Pan Pacific Suites Jijini Nairobi, wenyeji Singida Black Stars FC wamepangwa Kundi A pamoja na Garde Cotes FC ya Djibouti, Coffee SC ya Ethiopia na Polisi FC ya Kenya. ...

Simba yamtambulisha Seleman Mwalimu Gomez

Klabu ya Simba SC imethibitisha kumsajili mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomez’ kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca ya Morocco. Mwalimu (19) raia wa Tanzania aliyejiunga na Wydad mnamo Januari 2025, akitokea Singida Black Stars baada ya kuonesha kiwango bora wakati akiitumikia Fountain Gate FC kwa mkopo kutoka Singida Black Stars na kufunga magoli 6 kwenye nusu ya kwanza ya msimu wa 2024/25.

SIMBA KUWAAGA BOCCO, MKUDE NI DHIHAKA AU MAPENZI

Na Prince Hoza Matua  SEPTEMBA 10 klabu ya Simba SC inaadhimisha tamasha lake ya Simba Day katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, katika siku hiyo Wekundu wa Msimbazi watacheza mechi ya kirafiki na timu ya Police FC ya Kenya. Police FC ni mabingwa wa nchi hiyo na watawakilisha taifa hilo katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika kama ilivyo kwa Simba SC ambao wamemaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu bara msimu uliopita. Katika tamasha hilo Simba SC watatumia nafasi hiyo ya kutambulisha jezi mpya, wachezaji wa kikosi chake cha msimu ujao na pia safi yake yote ikiwemo makocha. Simba SC pia watatambulisha vikosi vyake vya timu za vijana kwa maana under-17 na under-20 pia timu ya wanawake, Simba Queens ambayo nayo imefanya usajili mkubwa kama ilivyo timu ya wanaume. Kitu ambacho kinanifanya niandike makala hii ni kitendo cha klabu hiyo kuwaaga wachezaji wake wawili wa zamani wote wakiwa manahodha, John Raphael Bocco na Jonas Gelard Mkude. Wachezaji hao waliichezea Simba kwa maf...

Namungo yapata mwarobaini wa mabao

Huenda Namungo inaenda kupata mwarobaini katika eneo lake la ushambuliaji ambalo msimu uliopita liliambulia kufunga mabao 28 tu katika #LigiKuu , Ongezeko la Rashid Mchelenga ambaye wamemnasa msimu huu kutoka Rwanda kunako klabu ya Musanze na Heritier Makambo kutoka Tabora united huenda likapunguza ufinyu wa upatikanaji wa mabao 2025/26. Mchelenga ana uzoefu na soka la Tanzania ambapo aliwahi kuitumikia klabu ya Pamba Jiji aidha Lipuli ya Iringa hata nje ya Tanzania amezitumikia klabu za Police Kenya na Musanze ya Rwanda si jambo Dogo! Rashid Mchelenga amerudi nyumbani kutoa ladha na hekaheka kwa wakazi wa Ruangwa na viunga vyake,

Jose Chameleone na mtaraka wake ngoma nzito

Mkongwe wa Mziki nchini Uganda Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone amevunja ukimya kuhusu mwenendo wa talaka yake na Mke wake Daniella Atim waliofunga ndoa miaka 17 iliyopita na kusisitiza kuwa  ingawa amekubali mali zake kugawanywa lakini hakubaliani na kitendo cha kulazimishwa kusaini wosia. Kwa mujibu wa ripoti ya Vyombo vya Habari Nchini Uganda vya BigEye na Pulse Uganda, Chameleone amesema hayo wakati akiwa LIVE kupitia kurasa zake Mtandaoni na kuweka wazi kuwa mali wanazogombea na Mkewe ni mali za Watoto na sio zao binafsi. “Mambo tunayopigania ni ya Watoto sio yetu na hata Watoto watawaachia Watoto wao, acha kutengeneza hali ambayo hakuna" amesema Chameleone. Mchakato wa kugawanywa kwa mali zake umeanza kuonekana mapema baada ya Mke wake kufungua mashtaka Mahakamani kudai talaka mnamo mwezi Machi mwaka huu ambapo August 21 alikubali kutoa talaka kwa kile Mkewe alichokiita kutelekezwa. Chameleone mwenyewe amesema kuwa hana pingamizi la kusaini hati za kisheria ikiwa ...

Rasmi, Simba yakataa kucheza Ngao na Yanga Septemba 16

“Kusema ukweli ukijaribu kuangalia ratiba imekuwa ngumu Sana  maana ratiba ya Ngao ni tarehe 16, kuanzia hapo tutakuwa na Siku tatu au nne inabidi tucheze mchezo wa ligi ya mabingwa Botswana, na kama unavyojua utaratibu wa kusafiri Botswana Huwa ni magumu sana na mara nyingi Huwa tunaenda na Ndege ya kukodi kuepusha usumbufu” Lakini ukijaribu kuangalia ucheze mechi tarehe 16, hapo hapo inabidi upumzike , halafu usafiri na baadae kati ya tarehe 19 au 20 ucheze Mchezo Unaweza kuona ni kwa Kiasi Gani ni vigumu” “Kama Mchezo utakuwa tarehe 20 angalau naona Kuna namna tunaweza kukimbizana na mambo lakini kama wenyeji wetu watachagua tarehe 19 basi ratiba itazidi kuwa ngumu zaidi” Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally akizungumza na E fm Leo.

Opah Clement kukinukisha LALIGA

Nahodha wa Timu ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars Opah Clement ametambulishwa kwenye kikosi cha SD Eibar inayoshiriki Ligi Kuu Hispania maarufu Liga F. Ametambulishwa kikosini hapo akitokea FC Juarez ya Mexico aliyoitumikia kwa msimu mmoja akicheza mechi sita kati bila ya kufunga bao wala asisti. Nyota huyo wa kimaaifa wa Tanzania anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na timu inayoshiriki ligi hiyo ambayo inashika nafasi yapili kwa ubora barani Ulaya.

Hatimayr Yanga yambakisha Clement Mzize

MSHAMBULIAJI Clement Francis Mzize ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga – baada ya klabu yake kuposti picha akiwa na Rais wa timu, Eng Hersi Said na kuambatanisha na ujumbe “Bado yupo sana. Mambo Uwanjani Blog ilikuwa ya kwanza kuwakilisha umma kwamba Mzize atabaki Yanga na sababu kubwa ni kumuongeza mkataba na kuboresha maslahi yake ambapo ilieleza kwamba Yanga itamlipa mshahara mkubwa ikitaja milioni arobaini na tano.

Simba na Yanga kuota mbawa

Awali mamlaka za soka ziliwambia Simba na Yanga kuwa ngao ingeweza kuchezwa kati ya tarehe 11-14 ila badae ratiba ikabadilika na mechi kupelekwa tarehe 16/09/2025. Now Simba wanasema mechi ikichezwa tarehe 16 wao hawatapata muda wa kujiandaa na mechi ya kimataifa dhidi ya   Gaborone Utd ya Botswana. Ikumbukwe mechi hiyo itapigwa tarehe 20/09/25 hivyo Simba wakimaliza ngao tarehe 16 kesho yake tarehe 17 watatakiwa kusafiri 3,411 km kwenda Gaborone kisha tarehe 20 kucheza mechi kubwa na ngumu kitu ambacho kwao kinawawia kigumu. Wao Yanga wako tayari kucheza ngao ya jamii coz mechi yao ya kimataifa ni tarehe 21 hivyo watapata siku tatu za kupumzika…..ila wao Yanga wanasema tofauti na tarehe 16 “HAWACHEZI”

Senegal yavuliwa ubingwa CHAN

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Senegal wametupwa nje ya michuano hiyo kufuatia kipigo cha penalti 5-3 dhidi ya Morocco katika katika dimba la Mandela, Kampala. Simba wa milima ya Atlas, Morocco wametinga fainali ya CHAN2024 ambapo watachuana na Madagascar iliyofikia hatua hiyo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan. Simba wa Teranga watachuana na Sudan kuwania nafasi ya mshindi wa tatu. Timu hizo ndani ya dakika 120 zilifungana 1-1 lakini mikwaju ya penalti ikatenganisha ambapo Senegal ikapata 3 na Morocco 5

Injinia Hersi amtembelea mzee Jabir Katundu

Rais wa Young Africans SC, Injinia Hersi Said leo amemtembelea Katibu wa zamani wa Klabu yetu, Mzee Jabir Katundu na kumkabidhi zawadi za jezi zetu mpya za msimu wa 2025/26. Mzee Jabir Katundu alikuwa Katibu wa Klabu ya Yanga miaka ya 1962-1966, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti Mohamed Mabosti. Hersi amemkabidhi Mzee Jarib Katundu, jezi zote za Klabu na kumuelezea maudhui yaliotumika kwenye ubunifu wa jezi hizo.

Mlandege yaiwahi Simba Septemba 27

Klabu ya Mlandege FC imewapiga bao Simba kwenye uzinduzi wa Jezi, Mlandege watazindua jezi zao tarehe 27 kesho Jumatano saa 12 Jioni ikumbukwe tarehe hiyo ilipangwa kuwa uzinduzi wa Jezi za Simba lakini wameghairisha mpaka tarehe 31.