Kiungo mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga, Mzambia Clatous Chama, amekamilisha usajili wa kujiunga na wawakilishi wa Tanzania bara katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, Singida Black Stars kwa kandarasi ya mwaka mmoja.
Tayari Chama alishaanza mazoezi na timu hiyo na usajili wake ni mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo Miguel Gamondi raia wa Argentina.
Ikumbukwe Chama na Gamondi walikutana Yanga msimu uliopita, Chama pia anaungana na Khalid Aucho na Nickson Kibabage.
Kila la kheri nyota hao ndani ya Singida Black Stars.